Unda, badilisha na ushirikiane na wengine kwenye mawasilisho kutoka katika simu au kompyuta kibao yako ya Android ukitumia programu ya Slaidi za Google. Ukiwa na Slaidi za Google unaweza:
- Kuunda mawasilisho mapya au kubadilisha wasilisho lolote lililopo
- Kushiriki mawasilisho na kufanya kazi pamoja na wengine katika wasilisho moja kwa wakati sawa.
- Kufanya kazi zako kutoka popote, wakati wowote - hata bila muunganisho wa intaneti
- Kuongeza na kujibu maoni.
- Kuongeza na kupanga upya slaidi, kubadilisha muundo wa maandishi na maumbo, na mengineyo.
- Kuwasilisha moja kwa moja kutoka kwenye kifaa chako cha mkononi.
- Kukaa bila hofu ya kupoteza kazi yako - kila kitu kinahifadhiwa kiotomatiki kadri unavyocharaza.
- Kuunda mawasilisho maridadi papo hapo kwa kutumia kipengele cha Kichunguzi.
- Kuwasilisha sladi wakati wa simu za video - mikutano iliyoratibiwa itaonekana kiotomatiki
- Kufungua, kubadilisha na kuhifadhi faili za Microsoft PowerPoint.
Taarifa ya Ruhusa
Kalenda: Inatumiwa kujiunga na simu za video kutoka kwenye mialiko ya kalenda.
Kamera: Inatumiwa katika hali ya kamera wakati wa simu za video na kuweka picha zilizopigwa kwa kamera.
Anwani: Inatumiwa kutoa mapendekezo ya watu wa kuongeza kwenye faili na wa kushiriki nao.
Maikrofoni: Inatumiwa kupitisha sauti wakati wa simu za video.
Hifadhi: Inatumiwa kuingiza picha na kufungua faili kutoka kwenye USB au hifadhi ya SD.
Ilisasishwa tarehe
12 Des 2024