Kwa mara ya kwanza, programu rasmi ya kupiga simu kutoka Google sasa inapatikana na inaweza kupakuliwa. Programu ya Simu hukusaidia kuwasiliana na jamaa na marafiki kwa urahisi, kuwazuia wanaopiga simu taka na kufahamu anayekupigia kabla ya kupokea simu – yote kwa muundo rahisi na wa kuvutia.
Ulinzi madhubuti dhidi ya taka
Utaona onyo kuhusu wapigaji simu wanaoshukiwa ili kukusaidia kuepuka simu usizotaka kutoka kwa wapigaji simu taka, wanaouza kupitia simu na walaghai. Zuia nambari ili wasikupigie tena.
Fahamu anayekupigia
Kipengele cha Google cha kitambulisho cha anayepiga simu ni cha kina na hukuwezesha kufahamu biashara inayokupigia simu ili uweze kujibu kwa ujasiri.
Chuja simu za wapigaji usiowajua 1,2
Kichuja Simu hujibu simu kutoka kwa wapigaji usiowajua, huwachuja na kuwaondoa wapigaji simu taka bila kukukatiza na hukusaidia kupata maelezo zaidi kuhusu wapigaji simu usiowatambua kabla hujapokea simu zao.
Ujumbe wa sauti unaoonekana 1,3
Angalia ujumbe wako bila kuhitajika kupiga nambari ya ujumbe wa sauti – angalia na ucheze ujumbe kwa mpangilio wowote, soma manukuu na ufute au uhifadhi ujumbe papo kwenye programu.
Muundo wa kuvutia
Muundo wetu rahisi na mwepesi hukusaidia kuwasiliana na watu uwapendao kwa kugusa mara moja tu. Vilevile, unaweza kubadili utumie hali nyeusi ili uokoe chaji na upunguze kuumiza macho wakati wa usiku.
Usaidizi wa Dharura 1,4
Ona mahali ulipo wakati unapiga simu ya dharura na umtumie mhudumu wa dharura maelezo kuhusu usaidizi unaohitaji pamoja na maelezo ya ulipo bila kuzungumza.
Programu ya Simu inapatikana kwenye vifaa vingi vya Android vinavyotumia Android™ 9.0 na matoleo mapya zaidi.
1 Inapatikana tu katika baadhi ya vifaa ambapo programu ya Simu imesakinishwa awali.
2 Kipengele cha kuchuja simu kiotomatiki kinapatikana nchini Marekani pekee, kwa Kiingereza pekee. Kipengele cha kuchuja simu mwenyewe kinapatikana nchini Marekani na Kanada pekee, kwa Kiingereza pekee. Kipengele cha kuchuja simu huenda kisitambue simu zote zinazopigwa na roboti au simu zote ambazo ni taka.
3 Kipengele cha Manukuu kinapatikana nchini Marekani pekee, kwa Kiingereza pekee.
4 Inapatikana nchini Australia, Uingereza na Marekani pekee, kwa Kiingereza pekee.
Ilisasishwa tarehe
12 Des 2024