Habari na karibu katika tovuti ya kutoa taarifa ya IWF Burundi
Tunajua kwamba kuona picha na video za unyanyasaji wa kingono kwa mtoto ni jambo la kuumiza. Tunataka ufahamu kuwa unapotoa taarifa kwetu unachukua hatua sahihi.
Taarifa yako inaweza kumuokoa mtoto muathirika kutoka katika unyanyasaji zaidi.
Kutoa taarifa ni kwa haraka na rahisi. Unaweza kutoa taarifa bila kujulikana. Kama ungependa kujua hatima ya taarifa uliyoitoa, tutahitaji barua pepe yako.
Tafadhali kumbuka: Kama ungependa kutoa taarifa zaidi kuhusu mtoto aliyepo kwenye mazingira hatarishi au taarifa nyingine yoyote tofauti na picha au video za ukatili wa kingono, tafadhali wasiliana na dawati la polisi karibu na wewe au piga simu namba 116, Huduma kwa Mtoto.