Ofisi ya Kimataifa ya Vipimo

Ofisi ya Kimataifa ya Vipimo (Kifar.: Bureau international des poids et mesures; Kiing. International Bureau of Weights and Measures) ni chama cha kimataifa mjini Paris chenye shabaha ya kutunza utaratibu wa vipimo sanifu vya kimataifa (SI).

Chanzo chake kilikuwa mapatano ya kimataifa kuhusu mita ya 1875.

Ofisi hufanya kazi yake chini ya kamati ya kimataifa ya vipimo. Kila baada ya miaka minne kuna mkutano mkuu wa vipimo (Conférence générale des poids et mesures) mwenye mamalaka juu ya maazimio yote kuhusu vipimo vya SI.

Ofisi inatunza kilogramu asilia ambayo ni mfano kwa mizani yote duniani. Inatunza pia mita asilia ingawa siku hizi elezo la mita haifuati teni gimba hili la metali bali fizikia.

Viungo vya nje

hariri