Nenda kwa yaliyomo

Ukuta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 08:34, 9 Novemba 2023 na AlvinDulle (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Kwa makala juu ya taasisi ya UKUTA, nenda UKUTA.

Ukuta wa matofali
Ukuta wa Berlin

Ukuta ni muundo wima unaopakanisha nafasi kuwa tofauti, kama maeneo ya ndani na nje au vyumba ndani ya jengo.

Ukuta nje ya jengo

[hariri | hariri chanzo]

Nje ya jengo ukuta hujengwa kwa kuonyesha mipaka ya eneo na kuzuia watu au wanyama kuingia ndani. Vivyo hivyo unaweza kulenga kuwazuia wasitoke. Katika matumizi haya ukuta unafanana na madhumuni ya fensi lakini ni imara zaidi.

Uwanja wa nyumba mara nyingi huzungushwa kwa ukuta kwa kuongeza usalama. Ukuta wa Berlin ulijengwa katikati ya jiji la Berlin wakati wa ugawaji wa Ujerumani ili wakazi wa sehemu chini ya utawala wa kidikteta upande wa mashariki wasikimbilie upande wa magharibi.

Katika mazingira ya ugomvi ukuta hujengwa pia kwa kuzuia mashambulio na kwa kusudi la kusaidia utetezi. Katika historia kuna mifano kadhaa ya kuta kubwa kama Ukuta wa China au kuta za mpakani wa Uajemi na Dola la Roma. Mara nyingi kwa kusudi hili miji ilizingirwa kwa ukuta (ngome).

Ukuta una matumizi tofauti tena kwa kuzuia banguko na miporomoko ya ardhi.

  • Kwenye mtelemko mkali ukuta unaweza kuzuia kuteleza kwa ardhi au mawe ya juu kushuka chini, mfano baada ya mvua, na kuharibu barabara au nyumba chini yake
  • Milimani ukuta unasaidia kuzuia uharibifu kutokana na banguko la theluji.

Ukuta ndani ya jengo

[hariri | hariri chanzo]

Ukuta ndani ya jengo huwa na madhumuni mawili:

Aina za maunzi ya kujenga kuta

[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina nyingi za maunzi yanayotumiwa kujenga kuta:

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukuta kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.