Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya
Mandhari
Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ilikuwa ushirikiano wa nchi za Ulaya katika mambo ya uchumi tangu 1958. Imekuwa chanzo cha Umoja wa Ulaya.
Jumuiya ilianzishwa na nchi sita za Italia, Luxemburg, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi na Ujerumani ya Magharibi katika mikataba ya Roma 25 Machi 1957 na kuanza kazi 1 Januari 1958.
Sababu muhimu za kuanzisha ushirikiano huo ilikuwa maarifa ya vita kuu ya pili ya dunia na nia ya kuzuia marudio kwa njia ya ushirikiano wa kiuchumi.
Jumuiya ilifaulu na nchi nyingine zilijiunga nayo:
- 1973: Uingereza, Ueire, Denmark (wanachama 9)
- 1981: Ugiriki (wanachama 10)
- 1986: Hispania, Ureno (wanachama 12)
Tangu 1991 Jumuiya iliendelezwa kuwa Umoja wa Ulaya.