Saidia kuboresha mustakabali wa Google
Tunathamini maoni yako
Tungependa kupata maoni yako, ili tuendelee kubuni bidhaa za Google zinazokufaa. Utapata nafasi ya kuchangia kwenye vitu ambavyo mamilioni ya watu hutumia kila siku, kuanzia barua pepe na programu za kuongeza tija hadi zana za wasanidi programu na waelimishaji.
Hata kama hutumii bidhaa za Google kwa sasa, bado unaweza kujisajili ili upate fursa ya kushiriki katika utafiti wetu. Iwapo mojawapo ya tafiti zetu unakufaa, tutawasiliana nawe kwa kukupa maelezo na hatua zitakazofuata. Washiriki wengi watapokea zawadi ndogo ya shukrani.
Ufuatao ni utaratibu wa kushiriki
Jisajili
Tupe maelezo kiasi kukuhusu kwa kujaza fomu. Yatatusaidia kubaini ikiwa tafiti zozote zijazo za UX zitakufaa.
Jiunge kwenye kipindi cha utafiti
Iwapo utafiti unakufaa, utapokea dodoso ya ufuatiliaji na maelezo kuhusu mada ya utafiti, ikiwa ni pamoja na hatua zitakazofuata na mahali.
Kubali shukrani zetu
Baada ya kukamilisha utafiti, washiriki wengi watapata zawadi ndogo ya shukrani kwa muda wao.