Nenda kwa yaliyomo

Junipero Serra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Junipero Serra alipokuwa na umri wa miaka 61 (1774).

Junipero Serra, O.F.M. (jina la kiraia lilikuwa Miquel Josep Serra i Ferrer; Petra, Majorca, Hispania, 24 Novemba 1713 - misheni ya San Carlos Borromeo de Carmelo, California, Hispania Mpya, leo nchini Marekani, 28 Agosti 1784) alikuwa mtawa, padri na mmisionari wa Kanisa Katoliki.

Alianzisha misheni moja katika Baja California na nyingine 9 kati ya 21 za kwanza kati ya San Diego na San Francisco, Marekani. Walengwa wakuu wa misheni hizo walikuwa Waindio, ambao aliwainjilisha kwa lugha zao pamoja na kutetea kwa nguvu haki za maskini, bila kujali matatizo na magumu mengi[1].

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 25 Septemba 1988, halafu na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 23 Septemba 2015.[2]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Agosti[3] au 1 Julai [4].

Sanamu ya Junípero Serra akiwa na Juaneño, mtoto Mwindio), Havana, Cuba.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake

[hariri | hariri chanzo]
  • Writings of Junípero Serra, ed. and trans. by Antonine Tibesar, 4 vols. (Washington, D.C,. 1955-66).
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/60125
  2. "Pope to Canonize 'Evangelizer of the West' During U.S. Trip". National Catholic Register. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-27. Iliwekwa mnamo 21 Januari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Martyrologium Romanum
  4. "Patron Saints and their feast days". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-06-22. Iliwekwa mnamo 15 Juni 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.