Kisahani cha uongezekaji
Mandhari
Kisahani cha uongezekaji (Kiingereza: accretion disk) ni muundo unaofanywa na maada imesambaa kwenye njiamzingo kuzunguka kiolwa chenye tungamo sana kitovuni. Kiolwa kitovuni mara nyingi huwa nyota. Msuguano, mnururisho usio sawa, athari mwendomajisumaku, na kani nyingine hupungua uthabiti na huangukisha maada kuelekea kiolwa kitovuni. Marudio zitokezazo ya mnururisho hutegemea tungamo ya kiolwa kitovuni. Visahani vya uongezekaji vya nyota changa na nyotaasili hunururisha pote pa mialekundu; vile vinavyozunguka nyota nutroni na shimo jeusi hunururisha miali-X. Sayansi ya mibembeo katika kisahani cha uongezekaji huitwa elimu tetemekokisahani.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kisahani cha uongezekaji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |