Nenda kwa yaliyomo

Mtandao wa kijamii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mtandao wa kijamii au mitandao ya kijamii ni wavuti au huduma ambapo watu huongea, au hujumuishwa pamoja na watu wengine aidha ndani ya nchi au ulimwenguni kote. Huduma ya mitandao ya kijamii inaweza kuunganisha watu wenye shauku/mapenzi ya aina moja (kama vile mpira wa miguu, shule, ndondi, vyakula vya aina mbalimbali, filamu, dini na kadhalika) pamoja na urafiki.

Sehemu kubwa ya mitandao ya kijamii inakupa fursa ya kutengeneza taarifa zako katika ukurasa wako ikiwa ni pamoja na picha na maelezo kiasi kuhusu wewe mwenyewe, hasa yale ya msingi: unaishi wapi, una asili ya wapi, elimu, unapenda nini na kadhalika.

Mitandao ya kijamii ilianza kupendekeza tangu hatua za awali za uvumbuzi wa wavuti wa Walimwengu kwenye mwaka 1993.[1] Baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu sana ni pamoja na Facebook, Instagram, Twitter na JamiiTalk kwa Tanzania inasaidia kuongeza kasi ya mawasiliano ulimwenguni. Hata matumizi ya simu za mkononi zimeanza kupungua umaarufu wake hasa kwa mtindo wa uharaka wake wa kupeana jumbe kupitia mitandao hiyo.

Mitandao ya kijamii inatumika kuwaleta watu pamoja na kujenga urafiki miongoni mwao. Mitandao ya kijamii inatumika kupeana taarifa na watu wengine. Matumizi zaidi ya mitandao ya kijamii yanaendelea kuvumbuliwa katika nyanja tofauti ikiwemo elimu[2][3], biashara, matangazo ya kibiashara, siasa[4], ajira[5][6][7], afya na matibabu[8][9], utawala[10][11] na kadhalika.

Mitandao mingi ya kijamii inapatikana katika simu za mikononi hasa zile simujanja. Kuna baadhi ya makampuni yanafungia uwezo wa kuingia katika mitandao ya kijamii hasa kwa malalamiko ya kwamba waajiriwa wanapoteza muda mwingi katika mitandao hiyo.

Oroha ya mitandao ya kijamii

[hariri | hariri chanzo]
  1. The Network Nation 2 by S. Roxanne Hiltz and Murray Turoff (Addison-Wesley, 1978, 1993)
  2. Lori Wade. "How Social Media is Reshaping Today's Education System". Center for Social Impact Communication (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  3. Khanyie Dlamini (2017-07-20). "The Role of Social Media in Education". LCIBS - London College of International Business Studies (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-26. Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  4. The Nieman Foundation for fairness in investigative reporting. "Social Media in Politics - Twitter and Facebook as Campaigns Tools". ThoughtCo (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  5. Ben Young (2018-05-16). "The Impact of Social Media On Employment: The Good, the Bad, and the Ugly". React at Cornell University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  6. National Association of Colleges and Employers Staff (2017-12-11). "The Role of Social Media in the Job Search". National Association of Colleges and Employers. Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  7. Jonathan A. Segal (2018-04-11). "LEGAL TRENDS Social Media Use in Hiring: Assessing the Risks". SHRM (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  8. The University of Scranton (2013-09-17). "Top 5 Ways Social Media is Used by Healthcare Professionals". The University of Scranton Online (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-03. Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  9. Smith, Stephen W.; Sherbino, Jonathan; Ennis-O'Connor, Marie; Haymond, Shannon; Carley, Simon; Berkwits, Michael; Saenger, Amy K. (2018-09-01). "The Power of Social Media in Medicine and Medical Education: Opportunities, Risks, and Rewards". Clinical Chemistry (kwa Kiingereza). 64 (9): 1284–1290. doi:10.1373/clinchem.2018.288225. ISSN 0009-9147. PMID 29789353.
  10. Evie Browne (2015-01-01). "Social media and governance". GSDRC (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-03. Iliwekwa mnamo 2019-06-03.
  11. Hootsuite (2019-02-25). "Social Media in Government: Benefits, Challenges, and How it's Used". Hootsuite Social Media Management (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-06-03.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.