Rahabu
Rahabu (kwa Kiebrania רָחָב Raẖav au Rāḥāḇ, maana yake "mpana") alikuwa mwanamke wa Yeriko wakati ambapo Waisraeli, wakiongozwa na Yoshua, walivamia nchi ya Kanaani katika karne ya 13 KK.
Kitabu cha Yoshua (2:1-7) kinasimulia jinsi huyo kahaba alivyokaribisha wapelelezi wawili wa Israeli, alivyowaficha wasikamatwe na wenyeji, na alivyowadai wamuapie watamuokoa pamoja na familia yake Mungu atakawapowajalia kuteka mji huo.
Ingawa Rahabu alifanya kazi haramu akasaliti mji wake, anasifiwa na Barua kwa Waebrania (11:31) kwa imani yake iliyomuokoa na kumuingiza katika taifa la Mungu. Pia anasifiwa na Barua ya Yakobo (2:25) kama kielelezo cha mtu anayetenda mema.
Rahabu (kwa Kigiriki Ῥαχάβ, Rakhab) anatajwa na Injili ya Mathayo (1:5) katika kitabu cha ukoo cha Yesu.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Rahab Ilihifadhiwa 14 Novemba 2007 kwenye Wayback Machine. at Ask Moses .com
- questions Ilihifadhiwa 8 Septemba 2019 kwenye Wayback Machine. about Rahab's actual profession.