Nenda kwa yaliyomo

Santa Cruz de Tenerife

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jiji la Santa Cruz de Tenerife
Nchi Visiwa vya Kanari
Provincia Tenerife
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 217.415
Tovuti:  http://www.sctfe.es/
Mji wa Santa Cruz de Tenerife
Eneo la Santa Cruz kisiwani

Santa Cruz de Tenerife au kwa kifupi Santa Cruz (Kihispania: Msalaba Mtakatifu) ni makao makuu ya utawala wa kisiwa cha Tenerife na moja kati ya miji mikuu miwili ya funguvisiwa la Visiwa vya Kanari inayojitawala ndani ya Hispania. Visiwa vya Kanari vimo katika sehemu ya Kiafrika ya Atlantiki.

Mji ulikuwa na wakazi 217.415 mwaka 2002. Uko kwenye kaskazini ya kisiwa cha Tenerife. Bandari ni kitovu cha kihistoria ch mji. Kuna feri kati ya mji na Las Palmas de Gran Canaria.

Santa Cruz ilianzishwa mwaka 1494 Wahispania walipovamia Tenerife na kufanya vita dhidi ya wenyeji. Mahali pa mji wa sasa kiongozi Mhispania alisimamisha msalaba mkubwa wa ubao aliposheherekea ushindi juu ya Waguanche wenyeji. Mji mpya ulipokeajina kutokana na msalaba huo.

Mji ulikua kama kituo muhimu cha safari za kuvuka Atlantiki kati ya Ulaya na Amerika.

Santa Cruz ilikuwa mji mkuu wa funguvisiwa mnamo 1812. Tangu 1982 ni mji mkuu pamja na Las Palmas de Gran Canaria. Kila baada ya miaka minne mmoja kati ya miji hii miwili una nafasi ya kuwa mji mkuu.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Santa Cruz de Tenerife kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.