Yohane Climacus
Yohane Climacus (kwa Kigiriki Ἰωάννης τῆς Κλίμακος, yaani Yohane wa Ngazi; 525 - 606) alikuwa mmonaki katika monasteri ya Mlima Sinai.[1] Ni maarufu kwa maandishi na miujiza yake.
Toka zamani anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Machi[2].
Kitabu cha Ngazi
[hariri | hariri chanzo]Habari za maisha yake ni chache, lakini tuna kitabu chake Κλῖμαξ (Ngazi)[3] na kingine kifupi zaidi Kwa Mchungaji ambacho ni kama nyongeza yake.[4]
Humo Yohane anasimulia namna ya kuinua roho na mwili wetu kwa Mungu kwa kujipatia maadili, akitumia ndoto ya ngazi aliyoiona Yakobo-Israeli kama fremu ya kutolea mafundisho yake ya kiroho.
Kila sura inahusu "kidato" kimoja, yaani mada moja. Jumla ya vidato vyote vya ngazi ni 30. Saba vya kwanza vinahusu maadili ya msingi kwa maisha ya juhudi. Vile 19 vinavyofuata (8–26) vinahusu ushindi juu ya vilema na upatikanaji wa maadili yaliyo kinyume chake. Vile 4 vya mwisho vinahusu maadili makuu yaliyo lengo la juhudi zote, hasa upendo (ἀγάπη).
Ingawa walengwa asili wa kitabu walikuwa wamonaki wa monasteri ya jirani, mapema Ngazi kikawa kati ya vitabu vilivyopendwa zaidi katika Ukristo wa mashariki, na kinasomwa sana, hata katika liturujia, hasa wakati wa Kwaresima Kuu kabla ya Pasaka.
Picha ya Ngazi
[hariri | hariri chanzo]Picha takatifu yenye jina hilohilo, Ngazi ya Kupanda kwa Mungu, inaonyesha ngazi ambayo kutoka duniani inafika mbinguni (taz Mwa 28:12). Wamonaki wengi wanaipanda; kileleni Yesu yuko tayari kuwapokea. Kuna malaika wanaowasaidia kupanda, na mashetani wanaojaribu kuwaangusha, hata kama wamepanda sana.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Mababu wa Kanisa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Zecher, Jonathan L. (2013), "The Angelic Life in Desert and Ladder: John Climacus's Re-Formulation of Ascetic Spirituality", Journal of Early Christian Studies, 21 (1): 111–136, doi:10.1353/earl.2013.0006, ISSN 1086-3184
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Duffy, John (2010), "Reading John Climacus: Rhetorical Argumentation, Literary Convention and the Tradition of Monastic Formation (review)", Journal of Early Christian Studies, 18 (1): 145–146, doi:10.1353/earl.0.0303, ISSN 1086-3184
- ↑ Stroumsa, Guy (2008), "The Scriptural Movement of Late Antiquity and Christian Monasticism", Journal of Early Christian Studies, 16 (1), Johns Hopkins University Press: 61–77, doi:10.1353/earl.2008.0011, ISSN 1086-3184
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- St John Climacus and the Ladder of Divine Ascent Sermon
- John Climacus: The Ladder of Divine Ascent By Colm Luibheid, John Henebry (Google Books)
- Excerpts from John Climacus Archived 22 Februari 2012 at the Wayback Machine.
- "St. John Climacus" article from The Catholic Encyclopedia
- St John Climacus (of the Ladder) Orthodox icon and synaxarion for Fourth Sunday of Great Lent
- Venerable John Climacus of Sinai, Author of "the Ladder" March 30 feast
- Pope Benedict XVI General Audience of Febr. 11, 2009 on John Climacus
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |