Saddam Hussein
Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti (28 Aprili 1937 - 30 Desemba 2006) alikuwa Rais wa Iraki, kuanzia tarehe 16 Julai 1979 hadi mwaka wa 2003, pia waziri mkuu wa Iraki kati ya 1994 na 2003.
Alipanda ngazi ndani ya serikali na chama cha Baath kama makamu wa rais aliyemtangulia Ahmad Hasan al-Bakr. Baada ya kupewa cheo cha rais aliua wapinzani wengi na kuimarisha utawala wake.
- Vita kati ya Irak na Uajemi (1980 - 1988) aliyoanzisha baada ya kuona jeshi la Uajemi lilidhoofishwa kutokana na mapinduzi ya Ayatollah Khomeini; alishindwa kufikia shabaha zake, akalazimishwa kukubali mkataba wa kusalimu amri na Uajemi.
- Vita ya Ghuba ya 1990/91 [1] alipoamuru jeshi la Iraki kuvamia nchi jirani ya Kuweit; hatua hii ilijibiwa na amri ya Umoja wa Mataifa Wairaki waondoke tena, walipokataa jeshi la kimataifa lililoongozwa na Marekani lilifukuza Wairaki katika Kuwait.
Ndani ya Iraki alipigania upinzani wa sehemu kubwa za wananchi hasa katika kampeni dhidi ya Wakurdi kaskazini mwa Iraki wakati wa vita dhidi ya Uajemi na dhidi ya Washia wa Iraki Kusini baada ya vita ya Ghuba.
Saddam Hussein aliondolewa madarakani wakati wa uvamizi wa Iraki na Marekani katika vita ya pili ya ghuba mwaka 2003. Alienda mafichoni kwa miezi kadhaa, akakamatwa na kupelekwa mbele ya mahakama ya Kiiraki iliyompa adhabu ya kifo kwa jinai dhidi ya binadamu na hasa kesi 148 za mauaji zilizothibitishwa mahakamani.
Alinyongwa Desemba 2006 katika kambi la kijeshi mjini Al Kadhimiya nchini Iraki.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saddam Hussein Profile by BBC News
- The Saddam Hussein Sourcebook Archived 13 Mei 2008 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Saddam Hussein kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ [1] Archived 8 Agosti 2008 at the Wayback Machine.[2]